TANZANIA YASHIKA NAMBA MOJA KWA KUPOKEA NDEGE ZA KIMATAIFA AFRIKA

Tanzania imechangia
asilimia 19.3 ya jumla ya wageni wa kimataifa waliofika
Afrika ikilinganishwa na Kenya iliyochangia asilimia 18.2, Misri
asilimia 17.2 na Afrika Kusini asilimia 12.1 kwa kipindi cha September
2016 hadi Januari 2017.
Hii ni kwa mujibu wa
ripoti mpya ya kampuni ya ufuatiliaji wa safari za anga ya FowardKeys
inayolinganisha data za safari za ndege kutoka shughuli zaidi ya milioni
16 kwa siku na msimamo wa Afrika katika ramani ya utalii duniani.
Ethiopia
imeporomoka kwa asilimia 4.0 kutokana na kupungua kwa wageni kutoka
ndani ya mataifa ya Afrika. Kiwango cha watalii kutoka Ulaya na
Mashariki ya Kati kimeshuka nchini humo , ikilinganishwa na kipindi kama
hicho mwaka jana.
Kikanda,
wageni waliofika katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
waliongezeka kwa asilimia 16.4 ingawa Ripoti inaeleza utoaji duni wa
huduma ya kuunganisha safari ndefu kama changamoto katika eneo hilo.
Kigali ilikuwa ni mji mkuu pekee kikanda kurekodi ukuaji kwa kiwango cha
tarakimu mbili na kuwa na uwezo wa safari ndefu kimataifa na zile za
ndani ya Afrika.
Kwa ujumla, kuna ongezeko la kiwango cha wageni wa kimataifa wanaofika Afrika kwa asilimia 10.3.
Estelle
Verdier, Mkurugenzi wa tovuti ya Jumia Travel inayojihusisha na
‘bookings’ za hoteli ambayo pia hivi karibuni ilianzisha huduma ya
kuuzia tiketi za ndege alisema ripoti ya ForwardKeys huonyesha ongezeko
la ukuaji wa safari za anga barani Afrika ambayo ni sambamba na ukuaji
wa utalii.
Msamaha
wa Viza Moroko, kuangaliwa upya vikwazo kutoka Afrika Kusini; na ndege
za moja kwa moja kwenda Kenya yalikuwa ni baadhi ya mambo kadhaa
yaliyochangia ongezeko la wageni kutoka Asia kwa asilimia 21.7
kimataifa.
ForwardKeys
inaonyesha asilimia 17.3 ya ukuaji wa ‘bookings’ za kimataifa barani
kwa nusu ya kwanza ya 2017 na kipindi hichi cha Pasaka ipo katika nafasi
ya kurekodi asilimia 53.1 ya ongezeko la jumla ya wageni waliofika
ikifuatiwa na ongezeko la asilimia 26.4 mwezi Juni.


