RAIS KENYATTA AWAOMBA RADHI WAKENYA KWA KUFUTWA UCHAGUZI WA CHAMA CHA JUBILEE

Rais
Uhuru Kenyatta amewaomba radhi wa Kenya kutokana na chama cha Jubilee
kujiandaa chini ya kiwango wakati wa kura za mchujo jana na kusababisha
kuhairishwa kwa zoezi hilo katika kaunti zote 21.
Akiongea
Ikulu, rais Uhuru amesema hakutarajia kujitokeza kwa wapigakura wengi
kiasi hicho, waliosababisha kuibuka kwa upungufu wa karatasi za kupigia
kura kwenye vituo vya kupigia kura.
Amesema
chama cha Jubilee kitaendesha uchaguzi huru na wahaki na kuongeza kuwa
yupo tayari kufuata matakwa ya wapigakura katika chaguzi za mchujo wa
wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu.


