WAZIRI MHAGAMA ASEMA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAMEKAMILIKA







Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha
sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano
Aprili 26, 2017.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.
“Nipende
kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya
Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia
mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri
Mhagama.
Amesema
sherehe hizo zitakuwa na upekee wa aina yake ukizingatia kuwa ni mara
ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
Akitaja
upekee huo, Waziri Mhagama amesema sherehe hizo zitapambwa na Gwaride
la heshima lililoandaliwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Maonesho ya
Kikosi cha Makomando, Onesho la Mbwa na Farasi waliofunzwa, onesho la
Ukakamavu la Uzalendo la Wanafunzi kutoka shule za Sekondari za Dodoma,
burudani za vikundi vya ngoma kutoka Kaskazini Pemba pamoja na Bendi ya
mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma, Yamoto Bend na Mwenge Jazz.
“Ikumbukwe
hii itakuwa mara ya kwanza kuiadhimisha sherehe hii ya Miaka 53 ya
Muungano wetu kwa kuzingatia Serikali sasa imeshahamia Dodoma na tayari
Watendaji wake wapo huku hivyo tuitumie fursa hii kuwaalika Wananchi
wote kuudhuria kwa wingi ili kuifanikisha na kuonesha Umoja
wetu.”Alisistiza Waziri
Kwa
upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) January Makamba ametoa wito kwa Watanzania wote wajitokeze
kwa wingi kwenda kuangalia mafanikio yaliyotokana na uwepo wa Muungano
huo.
“Muungano
huu umetupa mafanikio mengi ikiwemo; kuijengea nchi heshima, kuwepo kwa
Katiba, kuimarika kwa Taasisi za kimuungano, ongezeko la masuala ya
kimuungano kutoka 11 hadi 22, ongezeko la usalama, Kuwepo Mfumo dhabiti
wa kushughulikia changamoto za Muungano na ongezeko la ushirikiano kwa
masuala yasiyo ya Kimuungano.”Alieleza waziri Makamba.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana alipongeza jitihada za
Ofisi ya Waziri Mkuu hususan Kitengo cha Maadhimisho kwa kushirikiana na
Ofisi yake kwa kuratibu na kuhakikisha maandalizi yote yamekalika kwa
wakati uliopangwa.
“Niipongeze
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada zake kuiratibu siku hii muhimu kwa
Taifa letu, na nitoe wito kwa Wakazi wa Dodoma na walioko nje ya Mji
kuonesha mfano kuja kwa wingi ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.”Alisisitiza Mhe.Rugimbana.
CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZATATULIWA KWA KIASI KIKUBWA : MAKAMBA
CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZATATULIWA KWA KIASI KIKUBWA : MAKAMBA
Na; Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa - Dodoma
Waziri wa Nchi anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 kwaka huu 2017, Muungano unaotimiza miaka 53 wiki ijayo.
Waziri wa Nchi anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 kwaka huu 2017, Muungano unaotimiza miaka 53 wiki ijayo.
Waziri
Makamba amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na
waandishi wa habari ulioandaliwa na waratibu wa sherehe za kitaifa Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu na kusimamiwa
na Waziri Mwenye dhamana Mhe Jenista Mhagama.
Mhe.
Makamba amezitaja changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa
vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda
Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa swala hili
linafanyiwa kazi kwa kumalizwa kwa taratibu za kisheria.
Alisema
kuwa changamoto nyingine inahusu Hisa za Zanzibar kwa iliyokuwa bodi ya
safari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo ya tume ya
Pamoja ya fedha.
Awali
akizungumzia Muungano huo unaotimiza miaka 53, Waziri Makamba Alisema
kuwa umekuwepo kisheria na umerasimisha udugu na ushirikiano uliyokuwepo
kati ya Bara na Visiwani.
Mkutano huo wa waandishi wa habari uliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi hizo.
Mkutano huo wa waandishi wa habari uliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Rugimbana, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wa Ofisi hizo.


