Marekani Yaionya Korea Kaskazini Kutojaribu Jeshi lao
Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence
Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence ameionya Korea Kaskazini kutolijaribu Jeshi la Marekani akiahidi kwamba litatoa jibu lenye athari kubwa iwapo nchi hiyo itatumia silaha za kinyuklia.
Pence amesema utawala wa Rais Donald Trump utaendelea kufanya kazi bila kuchoka na washirika wake kama Japan, China na mataifa mengine yenye nguvu duniani kuweka shinikizo la kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskazini.
Makamu huyo wa Rais wa Marekani amesema Marekani kila mara itatafuta amani lakini chini ya utawala wa Rais Trump itakuwa tayari kujikinga na upande ambao utajaribu kuishambulia.
Pence na Waziri wa Ulinzi Jim Mattis wameonya kwamba jaribio la hivi karibuni la Korea Kaskazini kurusha kombora lililoshindwa lilikuwa tukio la hatari la uchokozi na kuwahakikishia washirika katika Bara la Asia kwamba Marekani iko tayari kufanya nao kazi kuhakikisha Rasi ya Korea haina silaha za kinyuklia.
Marekani Yaionya Korea Kaskazini Kutojaribu Jeshi lao
Reviewed by Unknown
on
8:27 PM
Rating: 5