Kesi ya inayomkabili Salum Njwete, maarufu ‘Scorpion’ ya
unyang’anyi kwa kutumia silaha imeahirishwa hadi Mei 2 mwaka huu,
kufuatia shahidi namba nane kwenye kesi hiyo kushindwa kufika mahakamani
hapo.
Kesi hiyo iliahirishwa Jumanne hii na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Wilaya ya Ilala, Flora Haule, kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali,
Cheses Gavyiole, baada ya Deus Magosa (45), ambaye ni shahidi wa nane
upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ya kumjeruhi kwa kumtoboa macho Saidi
Mrisho, kushindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kusumbuliwa na
maradhi ya shinikizo la damu na sukari.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga,alisoma maelezo ambapo kuna baadhi
shahidi huyo alikiri kuyatoa Polisi na mengine kuyakana na kudai kwamba
askari alimchukulia maelezo mara mbili, hatua ambayo iliilazimu
mahakama hiyo kuahirisha kusikiliza ushahidi huo hadi Aprili 18 (Jumanne
hii).
Inadaiwa kwamba Septemba 6, mwaka huu saa 4 usiku maeneo ya Buguruni
Sheli, Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Njwete alimjeruhi Said Mrisho na
kumuibia Cheni na fedha.
Kesi ya Scorpion Yapigwa Kalenda
Reviewed by Unknown
on
8:23 PM
Rating: 5