MABILIONEA TANZANIA WANUNUA KAMPUNI KUBWA YA MAFUTA AFRIKA

Mabilionea wawili raia
wa Tanzania Aunali na Sajjad Rajabali wamenunua hisa milioni 30.2 sawa
na asilimia 2.06 ya hisa zote katika kampuni ya mafuta ya KenolKobil.
KenolKobil ni kampuni
kubwa ya mafuta barani Afrika ambayo inajishughulisha na uuzaji wa
bidhaa hiyo katika nchi saba zilizomo Afrika Mashariki, Kati na Kusini.
Kampuni hii ilianzishwa mwaka 1959.
Kwa mujibu wa ripoti ya
mwaka iliyotolewa na kampuni hiyo, hisa hizo zina thamani ya shilingi
8.2 bilioni katika soko na kuwafanya Rajabali kuwa nafasi ya 9 kati ya
wawekezaji 10 bora wa kampuni ya KenolKobil.
Ndugu hao wawili mabilionea wamewekeza jumla ya TZS 15.1 bilioni katika kampuni mbili za Benki ya Ushirika na Kenol.
Wawili
hao wanafanya kazi kwa ukaribu na Benki ya CRDB nchini Tanzania na
uamuzi wao wa kununua makampuni hayo mawili makubwa unaonyesha wanaimani
na mafanikio ya kampuni hizo katika miaka ijayo.
Kampuni ya Kenol ilipata
faida ya TZS 52 bilioni kwa mwaka jana ikiwa imechangiwa na mauzo
makubwa, katika nchi inazofanya kazi pamoja na gharama ndogo za
uendeshaji.


