Akiongea
kwenye kipindi cha East Africa Breakfast Baba Levo amesema kata hiyo
ilikuwa haina maendeleo kutokana na kuwa chini ya CCM kwa muda mrefu
lakini toka kata hiyo imechukuliwa na upinzani chini yake saizi imepiga
hatua ndani ya muda mfupi.
"Kata ya Kigoma Kaskazini ilikuwa inaitwa Butiama kwa sababu toka
nchi hii imezaliwa ilikuwa inaongozwa na CCM sasa shida moja iliyoikuta
ile kata unakuta kiongozi anayeongoza ile kata ni CCM lakini Kigoma
Mjini yenyewe mara nyingi ilikuwa inaongozwa na madiwani wa upinzani,
kwa hiyo unajikuta ile Kata uwezo wa kupata maendeleo ni ngumu" alisema
Baba Levo
Mbali na hilo Baba Levo anasema wakati anakabidhiwa Zahanati hiyo na
CCM ilikuwa na uwezo wa kutibu Malaria tu na kupimisha uzito kwa watoto.
"Sasa hivi kata ya Mwanga Kaskazini imekuwa ndiyo bora kwa mkoa wa
Kigoma, imekuwa bora kwa sababu diwani wao nimetimiza ahadi zangu maana
mimi niliahidi ahadi saba tu, na kwa mwaka wangu wa fedha wa 2016/2017
nimetimiza ahadi tatu kwa hiyo katika miaka mingine iliyobakia natakiwa
kutimiza ahadi nne ambazo ni rahisi tu. Mimi wakati naipokea ile kata
nilikuta ina zahanati lakini zahanati ile ilikuwa inatibu Malaria peke
yake, kumbuka Zahanati ina kiwango cha magonjwa ambayo inatakiwa itibu
yakizidi mgonjwa aende hospitali kubwa lakini zahanati hiyo ilikuwa
inatibu Malaria peke yake na kupima uzito watoto kama kliniki sasa
nikajiuliza kama hii inahudumia watoto peke yake hii ni zahanati au
Chekechea ya watoto? alihoji Baba Levo
Baba Levo anasema toka amekuwa diwani saizi hiyo zahanati imekuwa
ikitoa huduma zote na kusema amezidi kuiboresha, kwa kuingiza maji,
kufunga umeme, pamoja na kujenga vyoo vizuri.