Kagera Sugar imefanikiwa kushinda 2-1
dhidi ya Simba kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara iliyofanyika
katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Simba ilionekana kutawala mchezo huo lakini wameshindwa kupata ushindi kwenye mechi hiyo kutokana na kutokuwa makini.
Goli la kwanza la Kagera Sugar limefungwa
na Mbaraka yusuf katika dakika 28 ya mchezo huo baada ya kupiga shuti
kali na kumshinda kipa wa Simba, Daniel Agyei na kutinga nyavuni.
Mshambuliaji Christopher Edward ndiye
aliyeshinda goli la pili baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa na beki
wa pembeni wa Kagera Sugar.
Goli la kufutia machozi la Simba
limefungwa na Mzamiru Yassin katika ya 60 ya mchezo huo baada ya piga
nikpige kwenye lango la Kagera Sugar.
Kwa matokeo hayo Simba anabakiwa na
pointi zake 55 akishika nafasi ya pili nyuma ya Yanga mwenye pointi 56
baada ya kushinda mechi ya jana dhidi ya Azam FC.
KAGERA SUGAR YAILIZA SIMBA KWA MABAO 2-1
Reviewed by Unknown
on
6:53 PM
Rating: 5