Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Muheza,
Rwebangira Mathias Karuwasha ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga
na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kutokana na chama hicho kupoteza dira
na mwelekeo.
Lakini kubwa zaidi
inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa kuiondoa uhalisi wa
chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea kuwa chama cha kuwa
mshindani na CCM ili kuleta mabadiliko.
Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza
kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa
viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya
Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama
hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.
Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake
na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo
Sahare Jijini Tanga,Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa
yaliyopelekea kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona
kuna sera makini zinazotekelezeka .
Amesema kutokana na matukio mbalimbali
anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei
kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa na watwana hivyo
nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera
makini na zenye mafanikio.
CHADEMA TANGA WAPATA PIGO....MWENYEKITI WA WILAYA YA MUHEZA AHAMIA CCM.
Reviewed by Unknown
on
7:01 PM
Rating: 5