Vikosi vya usalama
nchini Urusi wako kwenye taadhari kubwa baada ya kutokea milipuko kwenye
vituo viwili vya treni ya chini ya ardhi mjini St Petersburg.
Milipuko hiyo ilisababisha watu 11 kupoteza maisha na zaidi ya watu 40 walijeruhiwa.
Wachunguzi
nchini Urusi wamelichukulia tukio hilo kuwa ni shambulio la kigaidi.
Vyombo vya habari vimeripoti vikinukuu vyanzo vya usalama vikisema
milipuko hiyo huenda imelipuliwa na mtu aliyejitoa muhanga kutoka eneo
la Asia ya Kati.
Kifaa kingine kilichokutwa kwenye stesheni nyingine kiliteguliwa na wataalam wa kutegua mabomu.
Rais
Vladmir Putin yuko St.Petersburg kupata maelezo ya wataalam wa masuala
ya usalama, pia aliweka mashada ya maua kuwakumbuka walioathirika kwenye
ajali hiyo, amesema ni mapema mno kujua chanzo cha tukio hilo lakini
uchunguzi unafanyika.
''Sababu ya tukio hilo haijafahamika, hivyo
ni mapema kuzungumzia kuhusu hilo.uchunguzi utaonyesha , lakini maelezo
yote yatatizamwa, ilikupata sababu ya ajali hiyo na sababu ya uhalifu
huo, juu ya yote ugaidi, tutaona, uchunguzi utatupa majibu yote kuhusu
kilichotokea.'' alieleza Putin.
Aliyeshambulia Urusi anatoka Asia ya Kati
Reviewed by Unknown
on
8:24 AM
Rating: 5