Harmorapa Anusurika Kupondwa Chupa Akiwa Jukwaani.

Usiku wa Jumamosi hii Harmorapa amenusurika kujeruhiwa vibaya na chupa
wakati alipokuwa akitumbuiza katika ukumbi wa Maisha Basement uliopo
Kijitonyama katika usiku wa Komela.
Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio leo, meneja wa rapper
huyo Irene Sabuka amesema, Harmorapa alirushiwa chupa lakini kwa bahati
nzuri alikwepa la sivyo yangekuwa yanazungumzwa mengine.
“Kiukweli hili jambo la kusikitisha sana, Harmorapa alikuwa stejini ana
perfom ila kabla ya kumaliza show alitokea mtu mmoja akarusha chupa
stejini bahati nzuri Harmorapa alikwepa ile chupa. Laiti asingekwepa au
ingemkuta kwa bahati mbaya sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine,”
amesema meneja huyo.
“Mimi naona kile kitendo ni wivu tu sababu watu hawajui maisha kila mtu
ana namna yake anayotokea. Harmorapa ametokea mtaani anatafuta maisha
yake leo anaibuka mtu anamrushia chupa na kutaka kumjeruhi, anaibuka mtu
mwingine anasema kuwa anataka kumuonesha na kukomesha,” ameongeza.


