Polisi kwenye jimbo la Los Angeles nchini Marekani wanachunguza wizi
uliofanyika kwenye nyumba ya Nicki Minaj ambapo mali ya thamani ya
dola 175,000 iliibiwa.
Wizi huo ulitokea kwenye nyumba yake ya kifahari eneo la Beverly Hills lakini mwanamuziki huyo hakuwa nyumbani wakati huo.
Inaripotiwa kuwa nyumba hiyo ilivunjwa wakati wa uvamizi huo na baadhi ya nguo za Nicki Minaj kuibiwa.
Fanicha iliharibiwa huku picha na chupa za manukato zilivunjwa.
Bado haijulikani ni vipi waalifu waliingia nyumbani humo.
Waliiba vito vya thamani na bidhaa zingine zenye gharama ya dola 175,000.
Wezi wamfanyia Kitu Kibaya Nicki Minaj....Tazama Jinsi Alivyolizwa
Reviewed by Mipiko
on
9:41 PM
Rating: 5