Wachimbaji wa madini ya tanzanite wameunga mkono hatua ya
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusitisha fedha za ruzuku kwa wachimbaji ili
kuandaa utaratibu mpya utakaowezesha na wao kufaidika.
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Manyara (Marema),
Sadick Mneney alisema mchakato wa kupatikana kwa wanufaika wa ruzuku
hiyo inabidi upangwe upya kwa kuwashirikisha viongozi wa Shirikisho la
Madini Tanzania (Femata) wanaotambua matatizo yanayowakabili wachimbaji.
Alisema robo ya waombaji wa ruzuku hiyo wanatoka Mji Mdogo wa Mirerani
kwenye madini ya tanzanite, lakini wanashangaa hadi sasa hakuna
aliyepata.
Mneney alisema wachimbaji wa tanzanite wanatakiwa kuangaliwa kwa jicho
pevu, hivyo viongozi wa idara ya madini wanatakiwa kuwaeleza walipokosea
ili utaratibu mpya ukifanyika wapate fedha.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma alisema
mchakato wa kuwapata wachimbaji wa kupata ruzuku unafanyika kwenye ngazi
tofauti.
Juma alisema ili mchimbaji afuzu, anatakiwa kufuata vigezo ikiwamo
kulipa kodi, leseni isiyodaiwa, mgodi kufanya kazi, uzalishaji na kuwa
na namba ya utambulisho wa mlipa kodi.
Wachimbaji wa tanzanite wapongeza uamuzi wa Waziri Mkuu Majaliwa
Reviewed by Mipiko
on
7:34 AM
Rating: 5