Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 10
kwa wenyeviti wa mtaa mkoani kwake kuwataja watu wanaowahisi
wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Wito huo pia ni kwa watu
wote wanaohusika kwenye biashara hiyo haramu pamoja na wazazi
kuwasalimisha watoto wao.
Mkuu wa Mkoa huyo ameyasema hayo Jumatatu hii katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam akiongea na waandishi wa habari.
“Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es
salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya. Natoa siku 10
kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia
dawa za kulevya na unaishi naye, njoo utoe taarifa tukikukamata baada ya
siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikuwa sehemu ya
kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.”
Ameongeza, “Natoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za
kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekuwa ukifanya
biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo
tunao hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa
hamasa.”
Vita dhidi ya dawa za kulevya: Makonda atoa siku 10 kwa wahusika kujisalimisha
Reviewed by Mipiko
on
7:13 AM
Rating: 5