Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuna tatizo katika
usimamizi wa elimu visiwani humo kiasi cha kusababisha kuwapo kwa
matokeo mabaya kila mara.
Hayo yamesema na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali
Iddi alipokutana na viongozi wa shule na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali katika Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Balozi Idi amesema kamati za shule zina jukumu la kuondoa hali hiyo kwa
kuwabana walimu kila wanafunzi wanapofanya vibaya ili waweze kupandisha
kiwango cha ufaulu.
Amesema, kamati hiyo zinatakiwa kuwaita walimu na kuwaweka ‘kitimoto’
waeleze sababu badala ya kuwaangalia wakati jahazi la elimu
linaporomoka.
Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar amesema matokeo mabaya ya mitihani ya
wanafunzi yanadhihirisha usimamizi mdogo wa walimu shuleni
ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu, Riziki Pembe Juma amesema pamoja na kuwapo
kwa mikakati mbalimbali ya kiserikali kuinua elimu, wazazi wana nafasi
yao kufanikisha suala hilo na kwamba, walimu peke yao hawawezi
kufanikisha.
Riziki amewahamasisha wazazi na walezi kila mara wajitahidi kufuatilia mienendo ya watoto wao kuanzia shuleni hadi majumbani.
SMZ yachachamaa Kuhusu matokeo mabaya shuleni
Reviewed by Mipiko
on
7:54 AM
Rating: 5