Breaking News

Picha: Manji aonekana akitolewa polisi na gari la wagonjwa


Mfanyabiashara Yusuf Manji Jumapili ya jana alionekana akitolewa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi na kupandishwa kwenye gari la wagonjwa ambalo lilipita Barabara ya Sokoine kuelekea Posta Mpya.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, Manji alipanda gari hilo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lakini hawakufahamu mara moja alikoelekea.

Manji alikuwa amevaa fulana, suruali na viatu vya wazi vyote vya rangi nyeusi

Mwenyekiti huyo wa Yanga anashikiliwa na jeshi hilo kwajili ya mahojiano kuhusu tuhuma zinazomkabili za kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya.