Breaking News

AFYA YA TUNDU LISSU HII HAPA...AZUNGUMZA NA WATU, PIA AMEWEZA KULA

Ikiwa imepita wiki moja tangu kushambuliwa kwake, mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS)  Tundu Antiphas Lissu hii leo imearifiwa kwamba afya yake inaendelea kuimarika.

Akitoa taarifa hiyo kwa umma kupitia mtandao wa Twitter, mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Godbless Lema ameeleza kwamba Tundu Lissu anaendelea vyema na kuongeza kuwa leo ameweza kula vizuri na kuongea na watu.

"Mh. Lissu anaendelea vyema hospitali. Leo ameweza kula vizuri na kuongea na watu wengi zaidi....."aliandika Lema.

Aidha mbunge Godbless Lema amewashukuru watu wote ambao wamekuwa wakimwombea Lissu ili apone haraka huku akizidi kuwambea baraka za Mungu. Mh. Leama aliandika: "Ahsanteni kwa sala zenu. Mungu awabariki sana".

Mh. Lissu ambaye anaendelea na matibabu jijini Nairobi, Kenya alishambuliwa kwa risasi kadhaa na watu wasiojulikana siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita hali ambayo imemsababishia majeraha makubwa katika sehemu za mwili wake ikiwemo miguu, tumbo na mkono.