Breaking News

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU:ZIMBABWE YAANZA KIANDIKISHA WAPIGA KURA KWA MFUMO WA KISASA

Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe imeanza kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa biometric, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao.

Kwa mara ya kwanza Zimbabwe inatumia mfumo huo ili kupata idadi halisi ya wapiga kura, ikimaanisha kuwa hata wale waliojiandikisha awali wanatakiwa kujiandikisha upya. Zoezi la uandikishaji wapiga kura litaendelea mpaka Januari 15 mwakani.

Tume hiyo inatarajia kuandikisha wapiga kura milioni 7 kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka ujao, ikiwa ni ongezeko kutoka milioni 6.8 walioandikishwa katika uchaguzi wa mwaka 2013.