Rais wa Sudan kusini Salva Kiir amesema wanajeshi ambao wanawabaka raia wanapaswa kuuawa.
Ameyasema
hayo wakati alipotembelea mji wa Yei uliopo kusini magharibi mwa nchi
hiyo, ikiwa kama sehemu ya juhudi za upatanishi katika maeneo yenye
uhasama.
Kauli ya Rais Kiir ameitoa kufuatia tuhuma zinazotolewa
na makundi ya haki za binadamu kwamba wanajeshi wamekuwa wakiwabaka
wanawake.
Sudan kusini ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa
wenyewe mwaka 2013, baada ya Rais Kiir kutoka kabila la Dinka
alipomfukuza kazi Makamu wake Riek Machar kutoka jamii ya Nuer.
Ripoti
kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia nchini humo imeongeza hali ya
mvutano na wasiwasi kati ya serikali ya Sudan kusini na wafadhili kutoka
nchi za magharibi.
Rais wa Sudan Kusini ataka wanajeshi wabakaji wauawe
Reviewed by Mipiko
on
8:43 AM
Rating: 5