Leicester City imepanda mpaka nafasi ya
15 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuicha Liverpool
kwa mabao 3-1 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa King Power.
Leicester walionesha kiwango cha juu, na
magoli mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja kutoka kwa Danny Drinkwater
yaliididimiza Liverpool.
Wakicheza chini ya kaimu kocha Craig
Shakespeare, aliyechukua mikoba ya Ranieri, mabingwa hao wa England
walicheza kama mabingwa watetezi.
Goli la kwanza la Jamie Vadry
limekumbusha mtindo waliokuwa wakicheza msimu uliopita, baada ya pasi
murua kutoka kwa Marc Albrighton iliyomfikia Vardy.
Magoli haya ya Leicester ndio magoli ya kwanza kwa klabu hiyo kufunga mwaka huu wa 2017.
Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi
nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati
ya saba walizocheza katika michuano yote.
PL: Leicester City yailiza Liverpool 3-1
Reviewed by Mipiko
on
7:42 AM
Rating: 5