Serikali ya mkoa wa Mtwara imeendelea
kupokea misaada kwa ajili ya kusaidia baadhi ya watanzania walioondolewa
nchini Msumbiji kinyume na taratibu ili warudishwe makwao.
Akipokea msaada wa shilingi laki tano
kutoka kwa meneja wa benki ya Posta mkoa wa Mtwara, Mkuu wa mkoa huo
Halima Dendego amesema kuwa idadi ya watanzania waliorudishwa kutoka
Msumbiji imefikia 5634.
Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa kwasasa
idadi ya watanzania wanaotoka Msumbiji imepungua tofauti na kipindi cha
nyuma kutokana na wengi wao kurejea na kupelekwa makwao.
Pia Bi. Halima Dendego amesema kuwa
msaada huo utamfikia Agnesi Charles aliyeachiwa mtoto wa mwaka mmoja na
rafiki yake Jaquline Greyson ambaye alifariki dunia mara baada ya
kuingia nchini akiwa mgonjwa.
Wiki chache zilizopita watanzania
wamerudishwa kutoka Msumbiji kutokana na kuingia nchini humo bila vibali
maalumu vya kuishi katika nchi hiyo
Mtwara yapokea msaada kwa ajili ya Watanzania walioondolewa nchini Msumbiji
Reviewed by Mipiko
on
10:11 AM
Rating: 5