Msikilize Kamanda wa Polisi Dodoma Akiongea Kuhusu Kumkamata Zitto Kabwe Bungeni

Zitto
Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa Polisi wa bunge
wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye
hafahamu ni lipi
Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa amesema si kweli kwamba Polisi walikuwa Bungeni kumsubiri Zitto atoke wamkamate.
“Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae
“Unajua
watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe…
hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai” Amesema Kamanda Mambosasa.


