Kuna uwezekano kuwa wengi hawamufahamu Seven Mosha kama vile wanavyofahamika wasanii anaowasimamia kazi zao za muziki.
Seven Mosha akiwa na Alikiba
Jumapili, Feb 5, 2017 akiongea na kitengo cha Buzz kwenye gazeti kuu
nchini Kenya la Nation, Mosha alieleza kuwa alikuwa mtangazaji katika
kituo cha redio cha Clouds FM na pia kituo hicho kilipoanzisha label ya
kurekodi maarufu kama Smooth Vibe, alikuwa mhusika mkuu katika masuala
ya kusikiliza na kuandika muziki.
Alitoka Clouds FM mwaka wa 2009 na akajiunga na kituo cha televisheni
cha MTV ambapo anasema alihudumu kwa takribani miaka mitano toka
2005-2010 ambapo alikuwa katika kitengo cha ( Artiste and Repertoire)
maarufu kama A&R. Pia Seven alihudumu katika kampuni kubwa ya muziki
duniani ya Sony kwa muda kabla ya kusimamia tawi la Rockstar4000.
Seven Mosha anasema alizaliwa Nairobi Kenya lakini akahamia Moshi,
Tanzania. Familia yake ambayo iliishi katika mtaa wa kifahari wa
Lavington jijini Nairobi, ilihamia Tanzania akiwa na umri wa miaka minne
tu. Jina lake la kuzaliwa ni Christine Mosha lakini baada ya
kufundishwa kuhusu maajabu saba ya ulimwengu na dhambi saba kuu katika
dunia basi nambari saba ”Seven” ikawa nambari yenye nguvu katika maisha
yake na ndio maana akajiita Seven kama aka yake.
Aliliambia gazeti hilo kuwa, haamini kama anaitwa Christine, maana
kama angalikuwa na chembechembe za hulka la jina Christine, marafiki
zake wangelikuwa Elizabeth ama Victoria ambao wengi wao huwa wanategemea
mabwana zao kuwafanyia kila kitu katika maisha ilhali wakibaki kufanya
kazi za nyumbani kwa kimombo ”Housewives.”. Ni kilinukuu gazeti hilo, (She
does not believe she is a Christine,if she had a Christine character
her friends would be called Elizabeth or Victoria and she would a
housewife and stay at home).
Akigusia ushindani uliopo kati ya Diamond na Alikiba, Mosha
aliliambia gazeti hilo kuwa, anaamini ushindani katika tasnia ya
burudani ya muziki ni mzuri, kwasababu inawapa wasanii motisha ya
kuvalia njuga kazi zao na kutoa vitu venye ubora wa hali ya juu na
kuuikuza sanaa ya Afrika Mashariki katika viwango vya dunia.
Lakini akaongezea kuwa ataunga mkono ushindani kama huo pekee, pale
ambapo hautahatarisha maisha ya masanii yeyote yule. Bali anafurahia
vile Diamond na Alikiba wanavyoshinda kutoka production ya muziki hadi
kwa style za kimaisha.
Mosha aliongezea kuwa, huu ni mwaka wake wa sita tangu aanze kufanya
kazi na Alikiba. Na walikutana kwa mara ya kwanza katika project ya One8
ambapo katika project hiyo aliwasimamia wasanii wa Afrika Mashariki na
alisisitiza kuwa alipenda kila kitu kuhusu Alikiba. Baada ya project ya
One8 kuisha walikuwa wakiwasiliana na mwisho wakaamua kufanya kazi
pamoja. Pia Seven ni rafiki mkubwa wa Lady Jaydee, na picha ya macho
yake ndio yalikuwa kwenye cover ya album ya kwanza ya Lady Jaydee
”Machozi”.
Mkali wa Yahaya, Jide baada ya kutalakiana na mume wake ambaye pia
alikuwa manaja wake, Gardiner G Habash, alimuomba Mosha kusimamia kazi
zake za muziki na akakubali. Baadaye akakutana na Baraka The Prince
katika uzinduzi wa wimbi wa Alikiba, akamuuliza kama angekubali
kusimamia kazi zake na Baraka hakusita kukubali.
Gazeti la Daily Nation, linamuita malkia wa marejeo au kwa lugha ya
kizungu ( Queen of comebacks). Hii ni kwasababu ya uwezo wake
aliouonyesha, kuwarudisha kwenye game Alikiba akiwa na hit Mwana na
Jaydee ambaye alirudi kwenye muziki kipindi ambacho nyimbo zake zilikuwa
hazipati air play kwenye kituo cha redio cha Clouds FM ambacho ni
muhimu sana kwenye ku-support wanamuziki wengi nchini Tanzania kwasababu
za tofauti za kibinafsi ambayo baadaye ilitatuliwa.
Anasema hutumia pesa zake kwa kusafiri nchi tofauti tofauti za dunia,
na kila mwaka huenda nchi tatu tofauti ambazo huwa ni geni kwake.
Anapenda kupika na anapenda chakula kizuri pia.
Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : @ChangezN
Instagram: changez_ndzai