Mwanariadha wa Kenya,
Charles Maroa amefariki dunia kwenye hospitali ya KCMC iliyopo Moshi
baada ya kuanguka wakati akishiriki mbio za Kili Marathon zilizofanyika
jana mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kilimanjaro, RPC Willbrod Mtafungwa amethibitisha kutokea kifo hicho
kwa kusema kuwa mwanariadha huyo amekutwa na umauti majira ya saa tano
asubuhi katika hospitali ya KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.
Mwanariadha huyo
alianguka getini wakati akikaribia kumalizia mbio hizo zilizofanyika
jana na kushirikisha wanariadha mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi
ambapo kila mwaka hufanyika mkoani Kilimanjaro.
Baada ya kuanguka
alikimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu lakini alipofika
hospitali majaira ya saa tano asubuhi akafariki dunia.
Mashindano hayo
yalianza majira ya Asubuhi na kumalizika majira ya jioni ambapo
wanamuziki Joh Makini na Dogo Janja walipata nafasi ya kutoka burudani
kwenye mashindano hayo ya riadha.
Mbio za Kill Marathon zaondoka na Uhai wa mtu....Ni mwanariadha kutoka Nchini Kenya.
Reviewed by Mipiko
on
7:06 AM
Rating: 5