Kwa msanii au mtu maarufu, kinga pekee inayomsaidia
kuendelea kuwa na heshima yake, ni kuwa na wimbo unaofanya vizuri ama
kuwa na fedha.
Anapokosa hivyo, mambo hubadilika na hapo ndipo ule usemi wa Fid Q
kuwa usupastaa ni mzigo wa miiba huwa na maana. Hussein Machozi anaijua
hali hiyo na kupitia mitihani aliyopitia miaka miwili iliyopita,
amejifunza mengi.
“Nimejifunza kuna watu wa kweli na kuna watu feki,” Machozi ameiambia Bongo5.
“Kuna watu wa kweli ambao wamekaa na mimi kwa shida mpaka sasa hivi wapo
na mimi, marafiki wa kweli. Na kuna watu baadhi ambao walikuwa wapo
karibu sana na mimi kipindi nipo juu, lakini kipindi ambacho nilikuwa
kimya kwa muda mrefu, wameniacha mbali wamenitupa,” anasema.
“Wamenisahau,wameninyanyasa, imefikia kipindi wengine wanatongoza
mpaka mke wangu. Ni kitu ambacho kinauma sana na sio kwamba mtu
anamtongoza mtu hamjui, anamtongoza anajua kabisa huyu ndio future ya
Hussein Machozi, yaani ndio mtu anayemtegemea. Siwasemi wengine ni
mabosi walikuwa wanajifanya mabosi na vitu kama hivyo. Lakini yote
tupilia mbali, ni kwamba mimi nasonga mbele na maisha naendelea na
maisha yangu, nimesahau mabaya yote, nimefungua ukurasa mpya.”
Machozi ambaye kwa sasa anaishi nchini Italia amesema amenyanyuka
tena na sasa yupo tayari kurudi kwenye muziki. Anatarajia kuachia kazi
yake mpya iitwayo Nipe Sikuachi.
Hussein Machozi afunguka mengi Kuhusu msoto alioupitia....Awapa makavu marafiki feki...Bofya hapa
Reviewed by Mipiko
on
8:58 AM
Rating: 5