DITTO akwepa Soo La Dawa za Kulevya......asema yeye Hausiki.
Msanii
Lameck Ditto ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Moyo sikuma
damu' amefunguka na kusema yeye hausiki na biashara ya dawa za kulevya
wala matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaama amekosea kutaja jina.
Lameck
Ditto akiongea na EATV amesema kuwa hata yeye amesikia jina lake
likitajwa kwenye kundi la wasanii ambao wanahitajika kufika kesho kituo
cha polisi na kusema anadhani kuwa Mkuu wa Mkoa alikosea kutaja jina
lake.
"Kiukweli
mimi mwenyewe nimeshtuka sana maana sijihusishi kwa namna yoyote na
madawa ya kulevya, siuzi wala kutumia na siku zote nayapiga vita sababu
natambua si mazuri katika jamii, nadhani Mhe. alikosea kutaja jina maana
alisema Ditto lakini baadaye niliona amerekebisha na kusema Titto,
hivyo naomba Watanzania watambue mimi sihusiki na madawa ya kulevya"
alisema Lameck Ditto


