Maskini Weee… Snura alizwa na mwanaye ..!!!

MWANAMUZIKI wa miondoko ya
mduara, Snura Mushi, amefunguka kuwa amekuwa akilizwa kila mara na mtoto
wake wa kwanza Talha, kutokana na maneno anayomueleza kwa kitendo cha
baba yake kutompa huduma yoyote.
Akizungumza
Snura alisema kila mara mtoto wake anamuambia asikate tamaa ya kuwalea
na kumuombea kwa Mungu, aweze kumsaidia ili waendelee kusoma na kupata
huduma japo baba zao hawawajali yeye na mdogo wake kitu kinachomliza
mara kwa mara.


