Arusha: Lema 'Aendelea Kuongoza' Akiwa Mahabusu

Mambo yote yafanyikayo kwa kujadiliwa au kuamriwa na Baraza la Madiwani la Arusha ambalo linadhibitiwa na CHADEMA yanahusisha mawazo na melekezo ya Mbunge Lema. Taarifa zinaonesha kuwa Lema yu katika afya njema na mwenye ari kubwa ya kutenda kazi.
Lema, Mbunge wa kwanza wa upinzani jimbo la Arusha Mjini aliyeweza kutetea kiti chake cha Ubunge, anahusishwa na kuhusika na kila jambo jimboni Arusha katika kulipanga, kulijadili na kuliamua. Lema anatajwa kuwa ni mmoja wa Wabunge machachari wa upinzani nchini.
Yuko mahabusu baada ya kukosa dhamana katika mahakama huko Arusha katika kesi zake mbili za jinai. Bado Lema anapambania kupata dhamana huku akiendelea na kesi zake za jinai.


