Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na
kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini,
Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.
Baada ya mazungumzo hayo, Bi. Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe
wake wamelazimika kufika Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli kwa lengo
la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.
“Tumefarijika kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi
Rais Dkt Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki,
akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuiya hiyo kuona namna gani
wanaweza kutusaidia ili taifa la Sudan ya Kusini liwe taifa lenye amani.
Hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa
tunachokitaka ni amani katika nchi yetu na hiki ndicho kilio chetu, ”
alisema.
Naye Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa
Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia
ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa
taifa hilo.
“Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea
katika nchi ya Sudani ya Kusini hivyo ningezisihi pande zote
zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa
maendeleo ya taifa la Sudani ya Kusini,” alisema.
Sudan Yamwangukia Rais Magufuli...yamuomba kutatua mgogoro wao
Reviewed by Mipiko
on
6:52 AM
Rating: 5