Baada ya takriban wiki mbili kutokuwa machoni mwa watu, Kanye West ameonekana kwa mara ya kwanza.
Ameonekana Alhamis hii jijini Los Angeles katika eneo ambalo
hutengeneza vitu mbalimbali vya sanaa, Pacific Design Center. Katika
picha iliyowekwa kwenye mtandao wa TMZ, Kanye anaonekana akiwa amezipaka
rangi (blonde) nywele zake.
Rapper huyo alikuwa amelazwa kwa siku 10 hospitali kufuatia uchovu wa
kiakili na kuruhusiwa kwenda kuendelea na matibabu nyumbani. Tayari
imedaiwa kuwa ameanza kuandaa album yake mpya kupitia studio yake ya
nyumbani.
Wakati huo huo, rafiki wa karibu wa Kim Kardashian, amekanusha tetesi za mrembo huyo kutaka kuachana na Kanye West.
Kanye West aonekana kwa mara ya kwanza tangu atoke hospitali
Reviewed by Mipiko
on
7:31 PM
Rating: 5