Jeshi la usalama la Iraq jana limetwaa tena mtaa mmoja na vijiji
viwili, na kuwaua wapiganaji 200 wa kundi la Islamic State baada ya
askari wa jeshi hilo kuanza operesheni ya pili kuwaondoa wapiganaji wa
kundi hilo kutoka Mosul.
Askari wa kupambana na ugaidi wamewashambulia wapiganaji walioko
mstari wa mbele wa kundi la Islamic State kwenye mitaa kadhaa mashariki
mwa Mosul, na kuamua kuudhibiti mtaa wa al-Quds wakati mapambano makali
yanaendelea kwenye mtaa wa jirani.
Kwenye upande wa kaskazini, askari wa jeshi la Iraq walikomboa
kijiji cha al-Sada na kijiji cha Tawiyla na kupandisha bendera ya Iraq
kwenye jengo kuu baada ya kupambana vikali na wapiganaji wa kundi la
Islamic State.
Jeshi la Iraq lawaua wapiganaji 200 wa kundi la IS kwenye operesheni mpya ya kuukomboa Mosul
Reviewed by Mipiko
on
5:58 PM
Rating: 5