Rais Obama wa
ameamuru kutimuliwa kwa wanadiplomaisa thelathini na tano wa Urusi
kufuatia tuhuma za Urusi kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani
kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.
Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.
Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti
washtushwe na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu
mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa
upande wake, rais mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia taarifa hizo
za udukuzi, lakini hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa
Marekani ili kulijadili hilo.
Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa kiwango hicho hicho.
Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi
Reviewed by Mipiko
on
5:54 PM
Rating: 5