Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Bw. Ban Ki-moon amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais mtuele wa
Gambia Bw Adama Barrow, na kumwambia kuwa Umoja wa Mataifa unaiunga
mkono Gambia kufanya makabidhiano ya madaraka kwa wakati, kwa amani na
utaratibu.
Bw Ban Ki-moon amempongeza Bw Barrow kwa ushindi wake katika uchaguzi
wa urais, na kumtaka awahamasishe wafuasi wake wawe wavumilivu na
waepuke kuzusha vurugu.
Bw Barrow ameshinda katika uchaguzi uliofanyika tarehe mosi mwezi
huu, rais wa sasa Yahya Jammeh wa Gambia atakayemaliza muda wake tarehe
19 Januari mwakani alipinga matokeo siku chache baada ya uchaguzi huo.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeamua kutuma
vikosi nchini Gambia ili kulinda usalama wa rais mteule, viongozi wa
kisiasa na raia wa nchi hiyo.
Ban Ki-moon afanya mazungumzo na rais mteule wa Gambia
Reviewed by Mipiko
on
6:05 PM
Rating: 5