Afisa wa cheo cha
juu serikalini ameiambia BBC kwamba wasichana 21 waliokuwa miongoni mwa
wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram eneo la Chibok
sasa wako huru.
Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo
mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini
mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amethibitisha kuachiliwa huru kwa wasichana hao.
Bw
Mallam Garba Shehu ameandika kwenye Twitter: "Imethibitishwa kwamba
wasichana 21 wa Chibok wameachiliwa na kwa sasa wamo mikononi mwa Idara
ya Masuala ya Serikali."
Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.
Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.
Wapiganaji wa kundi hilo waliteka wasichana takriban 250 waliokuwa wakilala kwenye mabweni shuleni Aprili mwaka 2014.
Kisa hicho kilishutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Tangu wakati huo, ni msichana mmoja pekee aliyekuwa ameokolewa.
Kundi
la kujihami la wanakijiji lilimpata Amina Ali Nkeki mwezi Mei akiwa na
mumewe, ambaye anatuhumiwa kuwa mwanachama wa Boko Haram, pamoja na
mtoto wake.
Wasichana 21 wa Chibok 'waachiliwa huru' Nigeria
Reviewed by Mipiko
on
12:07 AM
Rating: 5