Mwanamapinduzi, Ernesto Che Guevara
Ernesto Che Guevara, rafiki wa chanda na pete wa
kiongozi wa mapinduzi ya Cuba, Fidel Castro, katika msitu ya Bolivia,
karibu na mji wa Higuera, kumelifanya jina la mpiganaji huyo wa chini
kwa chini lisife.
Kuuliwa hapo Oktoba 9 mwaka 1967 kwa Akiwa pamoja na wapiganaji
wenzake 17 waliochoka na kuvunjika moyo, Che Guevara alizungukwa na
wanajeshi 650 wa Bolivia pamoja na makachero wa Shirika la Ujasusi la
Kimarekani, CIA, akajeruhiwa kwa risasi, na maisha yake yakamalizwa
kabisa kwa kufyetuliwa risasi tisa na luteni wa jeshi aliyelewa. Julia
Cortez, mwalimu, alikuwa mtu wa mwisho kumuona Che bado yungali hai.
+
Naam alikuwa katika hali mbaya, kiafya, amekonda, nguo zinampwaya. Mtu
aliona vibaya kumuona katika hali hiyo, Lakini mtu aliweza kumtambuwa
kutokana na macho yake mazuri, mwili wake wote wa nje ulikuwa wa
kuvutia.+
Watu wengi, hata wale ambao walikuwa bado hawajazaliwa
wakati huo, wanalitukuza jina la Che Guevara na wanapata hisia ya
kutaka kuendeleza yale aliyoyapigania. Waliomuuwa Che Guevara walitaka
si tu mwili wake utoweke, lakini pia fikra zake, mtu aliyetambuliwa kuwa
ni mpiganaji wa uhuru. Maiti ilioneshwa kwa watu na kuchomwa moto
karibu na kiwanja kidogo cha ndege. Lakin kinyume na ilivofikiriwa, sura
ya mwanamapinduzi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 39 pale alipouliwa,
imebakia katika vichwa vya wapenzi na maadui zake.
Enzi za utoto wake
Ali Sultan, aliyewahi kuwa waziri katika serekali ya mapinduzi ya Zanzibar, anamkumbuka Che Guevara kama hivi:
Insert: Ali Sultan 1 ….
Pale kila mwamko wa fikra za siasa za kijamaa unapopata nguvu katika
Amerika ya Kati na Kusini, ndipo jina la Che Guevara linazdi
kuheshimika. Wale watu ambao sasa wanapinga utanda wazi wanamtathmini
Che kama mlezi wa fikra zao zenye kutetea maslahi ya walala hoi na
wanaoonewa katika mabara yote ya dunia. Pia Che Guevara limekuwa kwa
muda mrefu jina lenye kuvutia katika biashara ya mavazi, muziki wa aina
ya Pop, matangazo mengine ya biashara na alama ya maisha mbadala.
Kama
kamanda wa wapiganaji wa chini kwa chini huko Cuba, na ambayo mwaka
1959 yaliupinduwa utawala wa mdikteta Fulgigencio Batista, mzaliwa huyo
wa Argentina, pamoja na Fidel Castro ndio waliokuwa bongo nyuma ya
utawala mpya huko Havana. Che Guevara alikuwa hajashughulika kuwa na
cheo katika utawala huo mpya, lakini mwaka 1965 aliondoka Cuba na
kurejea katika mizizi ya harakati zake za kimapinduzi. Alijaribu
kuziwasha cheche za mapinduzi huko Kongo na baadae Bolivia.
Katika
nchi zote hizo mbili alishindwa. Huko Kongo alijaribu kuyasaidia
majeshi ya waasi, chini ya marehemu Laurent Kabila, yaingie madarakani.
Mbegu hizo za kimapinduzi alizotaka kuzipandisha Kongo, alifikiria
zitatoa matunda yake kwa kufanyika mapinduzi katika bara zima la Afrika.
Jee jaribio lake la Kongo lilishindwa? Ali Sultan, mtu aliyemjuwa vyema
Che Guevara, anasema Hata kidogo:
Insert: Ali Sultan 2
Baadae alielekeza nguvu zake huko Amerika ya Kusini na akifikiria kwamba
huko kutakuwa ni chimbuko la mapinduzi ya dunia. Aliitathmini vibaya
hali ya kisiasa na ya kijamii katika Bolivia, watu wa asili katika
maeneo hayo walimpa kisogo, huku jeshi la serekali pamoja na majasusi wa
Kimarekani wakizifuata nyendo za mwanamapinduzi huyo .
Che
Guevara alikuwa sio msuluhishi wa matatizo ya dunia hii, lakini alikuwa
mwananadharia ambaye fikra na vitendo vyake, kupitia haki aliyoiamini ya
kutumia nguvu na kuuwa, alitaka viamuwe mustakbali wa watu. Kikosi cha
wauaji wa Kipalastina ambacho mwaka 1977 kiliiteka nyara ndege ya
Shirika la Kijerumani la Lufthansa, ili kushikilia waachwe huru magaidi
wa jeshi jekundi la Ujerumani, RAF, walivaa flana zenye picha ya Che
Guevara. Washabiki wa Che Guevara walitamani ifike siku ambapo ustaarabu
wa kisiasa waliouchukia na ambao hawawezi wala hawataki kuishi ndani
yake utafutwa kabisa hapa duniani.
Vijana na wanafunzi wanaopinga
amri zozote za kutoka juu wanamuona Che Guevara na kumtukuza kama
mbadala wa uhuru. Tangu mwanzo alitaka kuweko udikteta safi wa chama
kimoja katika Cuba, jambo ambalo bila ya kujali lilipelekea sauti yeyote
ya upinzani kunyamazishwa.
Pale kiongozi wa Urussi, Nikita
Kruschov, aliporegeza kamba kutokana na mbinyo wa Wamarekani na kukubali
kuyaondosha maroketi ya kinyukliya ya masafa ya wastani ya nchi yake
kutoka Cuba, Che Guevara alimlaani kiongozi huyo wa Urussi kwa kuuridhia
ubeberu wa Marekani, na badala yake yeye alionyesha huruma yake kwa
wakoministi wa Kichina.Pale mwaka 1965 alipoilaumu wazi wazi Urussi,
Fidel Castro alikuwa hawezi tena kumstahamilia. Che aliondoka Cuba.
Baada
ya kushinda mapinduzi ya kikominsti ya Cuba mwaka 1957, Che Guevara
alichukuwa uongozi wa mahakama ya kimapinduzi ambayo iliwahukumu kwa
haraka maelfu ya watu walioitwa wapinzani wa mapinduzi na mamia yao
kupewa hukumu za vifo.
Ali Sultan, waziri wa zamani katika
serekali ya mapinduzi ya Zanzibar, hakubali kwamba Che Guevara alikuw
akatili mno kwa wapinzani wa mapinduzi ya Cuba:
Insert: Ali Sultan 3
Kama
waziri wa viwanda, mwaka 1961 alianzisha mpango wa uchumi wa mpangilio
na kulazimisha nchi hiyo ipige hatua za haraka kujenga viwanda na
kuzidisha uzalishaji wa miwa inayotoa sukari. Aliupinga sana ubinafsi
katika jamii ya Cuba.
Che Guevara alikuwa kama mwiba katika koo ya siasa ya nje ya Marekani. Tena Ali Sultan kutoka Zanziba:
Insert: Ali Sultan 4
Somo
gani Waafrika wanajifunza kutokana na maisha ya mtu huyo, aliyesomea
udaktari chuo kikuu, na mwishowe kuwa mwanamapinduzi na mopiganaji wa
misituni. Ali Sultan, mtu aliyemuona uso kw amacho Che Guevara anasema:
Insert: Ali Sultan 5
Mwaka 1977, mabaki ya Ernesto Che Guevara yalichukuliwa kutoka Bolivia na kuzikwa Santa Clara, Cuba.