Mwenyekiti wa Chama Cha wananchi CUF
anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim
Lipumba ametengua uteuzi wa wakurugenzi na manaibu wao sita kwa kile
alichokiita ni kutokana na changamoto zinazokikabili chama hicho.
Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao ni pamoja na Mkurugenzi wa
Uchumi na Fedha, Joran Bashange, wa Mambo ya Nje Ismail Jussa Ladhu,
Ulinzi na Usalama Mustafa Wandwi, na Haki za Binadamu na Sheria Kulthum
Mchuchuli.
Pia Prof Lipumba ametoa siku moja kwa wafanyakazi wote wanaofanya
kazi ofisi za CUF kwa kujitolea,kufika kesho Ofisini Buguruni kama
wanataka kuendelea kufanya kazi nae,na wale ambao watakaidi
kipufika,basi wajihasabie kuwa ndio wamejifukuzisha ktk nafasi zao
Meanwhile;Habari za watu wa karibu na Prof wanasema ameendelea
kulala na kushinda ndani ya Ofisi za CUF-Buguruni bila kutoka nje wala
wala mbali na eneo la ofisi hizo.Ni mwendo wa kulala na kuamka ndani ya
viunga vya Ofisi Buguruni.
Lipumba atimua Wakurugenzi Cuf
Reviewed by Mipiko
on
7:06 AM
Rating: 5