Brad Pitt na mtalaka wake Angelina Jolie wamefikia makubaliano ya muda
ambapo watoto wao sita watakuwa chini ya himaya ya mama na baba kupewa
nafasi ya kisheria kwenda kuwatembelea.
Makubaliano hayo ya wiki tatu yamewezeshwa na idara ya huduma ya jamii ya Los Angeles.
Katika
makubaliano hayo, kwa mujibu wa Us Weekly Jolie, 41, atakaa na watoto
hao sita: Maddox, 15, Pax, 12, Zahara, 11, Shiloh, 10, na pacha Knox na
Vivienne, 8 wakati mtalaka Pitt, 52,atapatiwa haki za kuwatembelea
watoto lakini katika ziara zake za kwanza ataangaliwa na therapist
ambaye atakuwa na mamlaka ya kumkubalia au kumkatalia kuona watoto.
Kitu kingine wawili hao watapatiwa ushauri wa kisaikolojia binafsi na baadae kifamilia wakiwa na watoto.
Kitu
kingine katika makubaliano hayo ni kwamba Pitt atakuwa bila
kutajhadharishwa kufanyiwa uchunguzi wa dawa za kulevya na pombe.
Imeelezwa kuwa uchunguzi wa kwanza dhidi yake alipita kwani hakukutwa na pombe wala dawa za kulevya.
Imeelezwa
kuwa Jolie amefurahishwa na mpango huo uliompa mamlaka kwa watoto na
sasa anataka kuwa nayo karibu kwa manufaa ya familia.
Jolie, aliomba talaka Septemba 19 akisema kwamba hawawezi kuendelea kuishi na mumewe kutokana na sababu zisizoweza kumalizwa.
Mshindi huyo wa tuzo za Oscar alidai talaka miaka miwili tu baada ya kufunga ndoa huku akiwa ameishi na Pitt kwa miaka 12.
Jolie , Pitt wafikia makubaliano, watoto kubaki na Jolie
Reviewed by Mipiko
on
6:47 AM
Rating: 5