"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima
kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala
pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini,
upendo penye chuki na heshima palipo na dharau "Baada ya kutamka
hayo mbele ya Mwl.Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa
Mwenge wa Uhuru.
Huyu Forojo Ganze,alikuwa ni mmoja kati ya
wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule Bagamoyo,
walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu
yeyote(Mwl.Nyerere), zindiko hilo lilifanyika Bagamoyo katika moja ya
mashimo yanayopatikana wilayani hapo,zoezi hilo lilienda sambamba na
kumuuliza shetani na malaika zake ni jambo gani lifanyike ili Tanzania
iendelee.Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia ktk hilo shimo kwaajili
ya kuuliza, alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha
wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee
wa Dar es salaam,kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi
hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha
isiyofahamika,wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba
hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere
alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha
juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii
115,kisha akakata roho.
-Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi
maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na
maana gani, baada ya hapo aliwagiza yahya Hussein atafasiri maana ya ile
namba 115, kama kawaida ya shehe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa
namba hiyo inamaanisha "utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la
Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38.Hii inamanisha
ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na
hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na
taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais
kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na
maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema,mbona haijawahi
kutokea rais akaongea na wazee wa bukoba jambo la kitaifa?,zindiko la
bagamoyo linafanya kazi. Safu hii ilikuwa ya watu 5 ambao ni. 1.mzee ramadhan,alizaliwa mwaka 1920 ,2.Ally tarazo(1929), 3.Komwe wa Komwe(1918) 4.Sheihe Yahya Hussein(1925),na 5.Forojo Ganze (1902)
JE, WAJUA NANI ALIANZISHA MWENGE WA UHURU???...TAZAMA VIDEO HII
Reviewed by Mipiko
on
7:40 PM
Rating: 5