DIAMOND PLATNUMZ ASEMA WATOTO WAKE WATAISHI AFRIKA KUSINI, KATOA SABABU HII
Sept 23, 2016 Diamond Platnumz alikuwa gumzo kwenye blogs mbalimbali na
mitandao ya kijamii baada ya kupost Nyumba ambayo aliandika kuwa ni
zawadi kuwa Mpenzi wake Zari.
Baada ya Diamond Platnumz kupost Nyumba hiyo ambayo iko South Africa
zikapita siku saba na akafanyiwa mahojiwa na kipindi cha Weekend Chat
Show cha Clouds Tv na kazitaja Gharama alizonunulia Nyumba hiyo.
Sasa basi.. Msanii wa muziki wa Bongo Flava Naseeb Abdul ‘Diamond’
ametoa sababu ya kununua nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 400
Afrika kusini, ni kwa sababu watoto wake wataishi nchini Humo.
Akiongea kupitia kipindi cha The playlist cha Times Fm Juzi Jumamosi,
Chibu amedai familia yake itaishi kwa Madiba kwa muda kadhaa.
“Watoto wangu wataishi Afrika kusini mpaka hapo baadae”. Alisema Diamond


