Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amekutana na
kiongozi wa upinzani ili kujadili jinsi ya kupata njia mbadala ya
kurejesha amani katika taifa hilo.
Mkutano huu unafanyika mara tu baada ya wapiga kura kupinga makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya serikali na waasi wa FARC.
Rais
huyo aliteua afisa mkuu kutoka serikalini ili kujali njia ambazo
zitaweza kuwasaidia kurejesha historia ya makubaliano ya amani na kundi
la FARC ambalo limekuwa katika mapambano ndani ya taifa hilo katika
kipindi cha nusu karne.
Rais wa zamani Alvaro Uribe wa nchi hiyo,
ambaye aliongoza kampeni ya kukataa makubaliano hayo hakuudhuria mkutano
huo na kuunda timu yake mwenyewe.
Rais huyo wa zamani anataka
waasi waliofanya uhalifu kuchukuliwa hatua kwa kuwekwa gerezani na
baadhi ya viongozi wa FARC kufungiwa kujihusisha na kisiasa.
Nae kiongozi wa FARC, Timochenko, anasema ataendelea kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa.
Colombia kujadili muafaka wa amani
Reviewed by Mipiko
on
4:08 PM
Rating: 5