Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist
cha Times FM, staa huyo alisema hiyo ni moja tu ya label kubwa za
Marekani alizozitolea nje. “Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata
wakitaka wanisaini,” alisema Diamond.
“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record
label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi,
wananifuata na ofa,” aliongeza.
“Lakini kila kitu ni target, mimi siku
yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under
record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza
kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata
collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo
sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo
ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”
Kingine Diamond alisema kama ni msanii mkubwa inakuwa rahisi kupata collabo za aina hiyo.
“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki
wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti
Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani
na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona
ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri.”
Diamond aeleza kisa cha kukataa kusainishwa na label ya Jay Z, Roc Nation
Reviewed by Mipiko
on
10:27 PM
Rating: 5