Breaking News

Waziri Ummy awatega wakurugenzi na waganga wafawidhi nchini




 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza kwenye maadhimish ya siku ya wazee Dunian ambayo kitaifa yalifanyikia Viwanja vya Shule ya msingi Ibar-Rujewa Wilaya ya Mbarali, Mbeya.
Wazee wakiwa katika maandamano kwenye maadhimisho yaSiku  ya Wazee ambayo kitaifa yamefanyikia Rujewa-Mbarali
kwanza kushoto ni wazir Ummya, katikati Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Mbunge viti Maalum, Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa.
Aah!! Hapo waziri Ummy akijaribu kupiga ngoma baada ya kuzawadiwa na wazee kutoka bonde la Usangu. Zawad hiyo iligawanyika ktika makundi matatu. Alipewa zawadi Waziri Ummy, Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Lengo ka kutoa ngoma hizo ni kwamba baada ya majukum mazito ya viongozi hao na wanapopumzika basi wanajifariji kwa kupiga na kucheza ngoma.

*Waziri Ummy Mwalimu atoa siku 90 kwa wakurugenzi na waganga wafawidhi nchin kuwatambua wazee na kuwapatia kadi za matibabu bure*

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  amewapa muda wa miezi 3 kuanzia jana kwa waganga wafawidhi na Wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutaumbua wazee wasio na uwezo na kuwapatia vitambulisho/Kadi za matibabu bila malipo.

Wazir Ummy alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye maadhimish ya siku ya wazee Dunian ambayo kitaifa yalifanyikia Viwanja vya Shule ya msingi Ibar-Rujewa Wilaya ya Mbarali, Mbeya.

Alisema  baada ya miezi mitatu atataka kuona wazee wote wasio na uwezo nchini wanapata huduma za matibabu bila usumbufu na kuulizwa barua za utambulisho kutoka Serikali za mitaa au vijijin.

*”Barua hizi zimekuwa ni kero kubwa sana na sehemu ya kuchangia vitendo vya udhalilishaji kwa wazee. Kwa hiyo suala hili ni kipaumbele kwetu. Hivyi mimi na wenzangu tutafanya ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa mikakati ya ustawi wa jamii wa wazee ili kuhakikisha wazee wanaondolewa kero zao na kujenga ustawi wa maisha yao*.

Mbali na hilo, Waziri Ummy alisema ili kutokomeza nankukomesha vitendo vya unyanyasaji na mauaji ya wazew na vikongwe,  Serikali inakusudia kupeleka  bungeni muswada wa Sheria ya Taifa ya Wazee kabla ya June mwakani ambao sio tu utaweka adhabu kali kwa wote watakaokitwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo bali utaweka wajibu wa kisheria kwa watoto ama familia kuwalea na kuwatunza wazee wao.