TID, Nature, Inspekta Haroun, Adili kusikika kwenye soundtrack ya ‘Karibu Kiumeni’
‘Karibu Kiumeni’ haitarajiwi tu kuja kuwa filamu ya Bongo yenye
mafanikio zaidi kuwahi kutokea, bali pia itakuwa filamu ya kwanza
iliyokutanisha mastaa wengi zaidi wa Bongo Flava kurekodi original
soundtrack yake.
P-Funk
Majani ndiye mtayarishaji mkuu wa soundtrack ya filamu hiyo
inayotarajiwa kutoka December mwaka huu. Soundtrack itajumuisha orodha
ndefu ya mastaa wa Bongo Flava
Karibu Kiume ni filamu iliyochezwa na Ernest Napoleon (Going Bongo),
Irene Paul, Idris Sultan na mastaa wengine na inatarajiwa kutoka
December mwaka huu.
Napoleon ameshare picha Instagram akiwa na waimbaji nguli wa Bongo
Flava watakaorekodi soundtrack hiyo inayosimamiwa na P-Funk Majani wa
Bongo Records.
Kutoka Kushoto: Inspekta Haroun, Adili, Ernest Napoleon, Juma Nature na P-Funk aliyekatwa
“#kiumenimovie all star soundtrack by #pfunkmajani loading
#jumanature #inspektaharun #tid #youngkiller #dogojanja #adili
#msagasumu #damiansoul,” ameandika Napoleon kwenye picha hiyo.
Wasanii watakaosikika ni pamoja na TID, Inspekta Haroun, Juma Nature, Adili, Young Killer, Msagasumu, Damian Soul na Adili.
Napoleon akieleza jambo. Pembeni yake ni Juma Nature
Crew nzima itakayohusika kupika soundtrack ya Karibu Kiumeni ikiwa nje ya studio za Bongo Records jijini Dar es Salaam
Kutoka Kushoto: TID, Rich One na Damian Soul
Kwenye picha hiyo juu, TID ameandika: We Back in Bussiness Once Again …Long Live MajaNi,Tanzania Need New Sound Fix this Problem


