Rapper wa kike Bongo, Chemical amefunguka kwa kuelezea
sababu inayomfanya afanye kazi nyingi na mtayarishaji wa muziki
Maximizer.
Akiongea na mtangazaji wa Radio Maisha ya Dodoma, Silver Touchez
kwenye kipindi cha Flavour Express, rapper huyo amesema Max amekuwa
akimpatia kwenye beat zake.
“Nina nyimbo nimefanya na maproducer wengine lakini nafanya nyimbo
nyingi na Maximizer kwa kuwa tumetoka pamoja kwahiyo nikienda naye mimi
nakuwa nasimama na Max naye anasimama na pia ni mtu ambaye ananipatia
sana. Ninaweza nikaenda kufanya kazi sehemu nyingine lakini nikiwa na
Max nakuwa poa,” amesema Chemical.
Rapper huyo ameongeza kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na Max kama baadhi ya watu wanavyofikiria.
Chemical afunguka sababu ya kufanya kazi nyingi na Maximizer
Reviewed by Mipiko
on
2:04 AM
Rating: 5