Naibu katibu mkuu wa Umoja wa
Mataifa Carlos Lopes amesema, Afrika haipaswi kutenganisha sekta za
uchumi, jamii na mazingira katika njia ya kujiendeleza.
Lopes ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Kamati ya Uchumi wa
Afrika kwenye Umoja wa Mataifa amesema hayo huko Lome ambako anashiriki
mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu mambo ya usalama wa bahari na
maendeleo. Amesema, serikali za nchi za Afrika, jumuia za kiraia na
wenzi wa ushirikiano wanapaswa kusukuma mbele maendeleo ya uchumi, jamii
na mazingira ya Afrika kwa wakati mmoja, na Umoja wa Mataifa unapaswa
kutoa msaada wa rasilamili.
Ameongeza kuwa uchumi wa Afrika upo kwenye mchakato wa
kubadilika, na kwamba sehemu kubwa ya ongezeko la uchumi huo inatokana
na ongezeko la soko la ndani, lakini ongezeko hilo halichangii mapato ya
serikali kutokana na kodi ya kiwango cha chini.
Bw. Lopes pia amezihimiza nchi za Afrika kuyaongezea kodi makampuni makubwa ili kukabiliana na upungufu wa misaada.