Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipokea
kiasi cha Shilingi Milioni 1.6 kutoka kwa Mratibu Taifa wa Mafunzo ya
Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi Bi.
Mariam Kilembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa ajili ya Kusaidia
wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, leo Bungeni Mjini Dodoma.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 121.679 ili kusaidia
wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera,
Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.
Msaada
huo umetolewa leo (Ijumaa, Septemba 16, 2016) na wadau mbalimbali
wakiwemo Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Caspian, Bw. Omid
Karambech aliyetoa sh. milioni 100.
Wengine
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bordar Limited, Bw. Wu Yahui
aliyetoa sh. milioni 20 pamoja na Bi. Mariam Kitembe aliyetoa sh.
milioni 1.679 kwa niaba ya Wauguzi walioshiriki mafunzo ya Utafiti wa
viashiria na matokeo ya ukimwi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Akipokea
msaada huo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Waziri Mkuu
amewashukuru kwa michango yao ya fedha na kuwaomba wananchi wengine
wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo
ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.
Jumapili,
Septemba 11, mwaka huu, Waziri Mkuu alifanya ziara mkoani Kagera ili
kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo pamoja na kujionea madhara
yaliyojitokeza.
Pia
aliongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba kuaga miili ya watu
16 waliofariki kutokana na tetemeko hilo. Aliwaomba wananchi wawe
watulivu na kuwaahidi kuwa Serikali itakuwa pamoja nao.
Jumanne,
Septemba 13 mwaka huu Waziri Mkuu aliongoza hharambee ya kuchangia
waathirika wa tetemeko hilo na kupokea zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa
mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa
Kitanzania.
Mbali na
kusababisha vifo, watu wengine 253 walijeruhiwa na maelfu ya wananchi
walikosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata
nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, SEPTEMBA 16, 2016
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MSAADA WA SH. MIL. 121.679
Reviewed by Mipiko
on
9:54 PM
Rating: 5