Tofauti ya Lugha yachelewesha kesi ya Ugaidi Mombasa
Kesi dhidi ya
wanawake watatu walioshukiwa kuhusika katika shambulio dhidi ya kituo
kimoja cha polisi katika mji wa bandarini wa Mombasa nchini Kenya
mwishoni mwa juma, ilishindwa kufanyika kutokana na matatizo ya
mawasiliano.
Mmoja wa washukiwa hafahamu kabisa Kiingereza au Kiswahili.
Shukri
Ali, ambaye ni mlemavu wa kutosikia, hakujibu lolote hata baada ya
mfasiri wa ishara aliyeletwa mahakamani kumsaidia kuelewa kesi dhidi
yake.
Mtafsiri wa lugha ya Kisomali pia alikuwa mahakamani ili
kuwasaidia washukiwa wawili, Saida Ali na Naima Mohamed Ali, ambao
hawana uwezo wa kufahamu KiingerezaJaji Emmanuel Mutunga, aliamuru Shukri Ali,
kupelekwa hadi katika wachunguzi maalum wa kimatibabu, katika hospitali
ya kitaifa ya Coast General.
Wanawake hao watatu, ambao bado wanazuiliwa pia watachunguzwa na madaktari.
Wanashtakiwa
kwa kosa la kuwapa hifadhi wanawake watatu wanaodaiwa kuunga mkono
kundi la Islamic State, ambao waliuwawa pale walipojaribu kushambulia
kituo cyha polisi cha Mombasa siku ya Jumapili iliyopita.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 21, wakati ripoti ya kimatibabu itakapowasilishwa mahakamani.