Wafanyakazi
wa Kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa
na kombe na cheti cha ushindi baada ya kiwanda hicho kutwaa tuzo ya
kuwa kiwanda bora na kushika nafasi ya kwanza Afrika kati ya viwanda 21
vya bia barani Afrika muda mfupi baada ya Meneja wa Kiwanda hicho,
Jemedari Waziri kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe
(SIA)-Mbeya akitokea Afrika ya Kusini.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakionyesha kombe na cheti cha
ushindi mitaani wakati wa mapokezi ya Meneja wa Kiwanda hicho.
Meneja
Rasilimali watu wa kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, Sarah Zayumba
(aliyeshika kombe), akiwa ameshika kombe hilo baada ya kuwasili katika
kiwanda hicho.
Kombe la Ushindi ambalo kiwanda kimetunukiwa
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiangalia kombe la ushindi
Baadhi ya wafanyakazi wakipata chakula katika hafla ya kusheherekea ushindi
Wakati
serikali ya awamu ya tano ikiweka mikakati ya kuifanya Tanzania nchi ya
viwanda tayari dalili njema zimeishajitokeza kuwa tukiamua tunaweza kwa
kuwa kiwanda kinachoshikilia rekodi ya ubora barani Afrika ni kiwanda
cha kutengeneza bia cha TBL kilichopo katika kitongoji cha Iyunga ndani ya Jiji la Mbeya.
Kwa mara nyingine, baada
ya kushindanishwa na viwanda vikubwa vipatavyo 21 barani Afrika,
mwishoni mwa wiki iliyopita TBL Mbeya imeibuka kinara na kutangazwa kuwa
kiwanda bora barani Afrika kati ya viwanda vilivyopo chini ya kampuni
kubwa yenye viwanda vya kutengeneza bia ya SABMiller na kulinda rekodi
yake ya kuwa kiwanda bora.
Rekodi
hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wa viwanda sio lazima ufanywe maeneo
ya mijini kama ambavyo ilikuwa imezoeleka kwa muda mrefu.
Akizungumzia
ushindi huo Meneja wa Kiwanda hicho, Mhandisi Jemedari Waziri, alisema
anajivunia ushindi huo kwani uthibitisho halisi kuwa watanzania tunaweza
kufanya vizuri na kuleta maendeleo kwa kasi tukiamua.
“Tunaposema
ubora wa kiwanda tunaamaanisha ubora wa bidhaa tunazozalisha,
teknolojia tunazotumia, raslimali watu tuliyonayo, mchango wa kiwanda
kwa Serikali na jamii iliyotuzunguka bila kusahau utunzaji wa mazingira
ambayo ni moja ya nguzo ya kampuni yetu”.Alisema.
Aliongeza
kuwa ushindi huu ni kwa wana Mbeya wote na wana kanda ya Nyanda za Juu
Kusini “Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kutuunga mkono wakati wote
na tutaendelea kuwaletea bidhaa bora kwenye soko na kubuni miradi
mbalimbali ya kijamii itakayosaidia kuleta mabadiliko”.Alisema
Jemedari
pia alisema ushindi huu unatokana na jitihada za pamoja kutoka kwa
wafanyakazi wote wa kiwanda na TBL Group kwa jumla na anafurahi kuona
kiwanda kinaendeshwa na watanzania asilimia kubwa ikiwa ni vijana
waliobobea katika fani mbalimbali.
TBL yavunja rekodi ya utengenezaji bora wa Bia barani Africa.
Reviewed by Mipiko
on
8:31 PM
Rating: 5