Spika wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amekabidhiwa
kitambulisho chake cha Taifa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu
Nchemba leo mjini Dodoma ambacho kinaonesha picha yake, saini yake
pamoja na saini ya mtoa kitambulisho.
Hatua
hiyo ya Spika Ndugai ya kupokea kitambulisho hicho ni mkakati wa taifa
ambao NIDA imekusudia kukamilisha usajili wa vitambulisho vya taifa nchi
nzima kwa wananchi, wageni na wakimbizi ifikapo Desemba mwaka huu
pamoja na kutoa namba ya utambulisho ambayo itawezesha makundi yote
kupatahuduma mbalimbali.
Ili
kufikia malengo ya usajili wa ya kusajili Watanzania milioni 24, NIDA
imekusudia kutumia taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) milioni
22.7 ambazo watachakatwa na kutoa namba ya utambulisho (NIN) kabla ya
kuzalisha kitambulisho cha taifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumkabidhi Spika kitambulisho
hicho, Waziri Mwigulu alisema kuwa kwa kutumia mfumo wa utambuzi na
usajili wa watu utasaidia kuwaunganisha wananchi na mifumo mingine ya
huduma ikiwemo mifuko ya hifadhi za jamii, benki, Bodi ya mikopo ya
elimu ya juu, RITA na TCRA pamoja na taasisi nyingine zinazotoa huduma.
Awali
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano NIDA Bi. Rose Mdami amemueleza Spika
Ndugai kuwa vitambulisho hivyo vinaenda sambamba na mfumo wa utambuzi na
usajili wa watu utakaowaunganisha na mifumo mingine muhimu hapa nchini.
Bi. Mdami
ameeleza kuwa mfumo huo umeunganishwa na Taasisi muhimu za Serikali
ikiwemo TAMISEMI, TRA, TCRA, TASO, NEC, MDA, RITA, Polisi Uhamiaji,
HELSB, Mifuko wa Hifadhi ya Jamii ili kuweza kuwa na taarifa za uhakika
kwa muhisika.
Amesema kuwa mfumo huo wa utambuzi utaisaidia nchi katika masuala ya usalama, kuweza kuwatambua.
Spika Ndugai akabidhiwa kitambulisho cha taifa
Reviewed by Mipiko
on
8:06 PM
Rating: 5