BAADA ya
meneja wa staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Best Naso kuwasiliana na
uongozi wa staa wa muziki kutoka Nigeria, Mr Flavour, good newz ni
kwamba, staa huyo amebariki kufanya naye kolabo.
Akichati na Showbiz Xtra kwa
njia ya WhatsApp moja kwa moja kutoka Nigeria, Meneja wa Best Naso,
Hamis Kibiti ‘Mbaba’ alisema kila kitu kinakwenda sawa na wamelazi-mika
kumtafuta msanii huyo kwa kuwa mashabiki wengi wa Best Naso wamekuwa
wakimfananisha naye kwa muonekano hadi kuimba.
“Mr Flavour ni msanii mtulivu na
muelewa, anaukubali sana Muziki wa Bongo Fleva na niwaambie tu mashabiki
wa Best Naso sasa watakuwa wamepata kile kitu walichokuwa wakikitamani
kifanyike,” alisema Mbaba.
Best Naso alishawahi kubamba na ngoma
kibao kama Yana Mwisho, Narudi Morogoro, Maisha Utata, Umedata, Rumba na
sasa anabamba na Ukweli Upo Wapi.